Mabingwa wapya wa Kagame Dar Young African,imemsajili Mshambuliaji wa Atletico ya Burundi, Didier Kavumbangu kwa ajili ya msimu wa ligi kuu unaotaraji kuanza hivi karibuni.
Kiongozi Mkuu wa Kamati ya Usajili ya
Yanga, Seif Ahmad 'Magari'
amesema wamemsajili mchezaji huyo kwa ajili ya kuimarisha safu ya
ushambuliaji yenye wakali wengine kama Hamisi
Kiiza na Said Bahanuzi.
Kavumbangu ndiye aliyefunga mabao yote mawili
katika mchezo wa kwanza wa Kundi C, Yanga ikilala 2-0 mbele ya Atletico,
mchezo pekee mabingwa hao wa Kagame kufungwa mashindano ya mwaka huu.
Yanga wamekuwa mabingwa baada ya kuichapa bila huruma wana lamba lamba Azam fc hiyo jana bao 2-0 na kufanikiwa kuongeza idadi ya vikombe vya Kagame
EmoticonEmoticon