LOGO YAMHAMISHA NGASA AZAM FC



Mshambuliaji wazamani wa Yanga na timu ya Taifa aliyepo Azam FC amesajiliwa na Wekundu wa Msimbazi Simba SC kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu ya Vodacom kwa uhamisho wa $50,000.

Ngassa ameitumikia Azam FC kwa misimu miwili ambapo ameweza kuwapa taji la Kombe la Mapinduzi mwaka 2012, kuwezesha Azam FC kushika nafasi ya pili katika ligi kuu ya Tanzania Bara msimu wa 2011/12 pamoja na Kagame Cup 2012 nafasi ya pili.


Taarifa iliyowekwa katika ukurasa wa Facebook wa Azam fc inaeleza kuwa klabu hiyo imefikia uamuzi huo baada ya Ngassa kuonesha dhamira ya kutotaka kuendelea kuitumikia klabu hiyo ya Chamazi baada ya kunaswa anaibusu logo ya wapinzani wakubwa wa Simba Yanga.


"Klabu ya Azam FC inapenda kutoa taarifa rasmi kuwa baada ya baada ya mchezaji wetu Mrisho Khalfan Ngasa kuonesha wazi kuwa na mapenzi na Yanga kwa kuivaa jezi na kuipiga busu Logo ya Yanga.

 Tuliwapa Yanga nafasi ya upendeleo ya kumnunua lakini hadi leo hakuna ofa iliyokuja toka Yanga.
 Simba wametoa ofa na uongozi unatafakari ofa ya Simba ,Ngasa anauzwa $50,000 wadau wa Yanga tunajua mnampenda sana Ngasa... fikisheni ujumbe kwa uongozi wenu, " ili eleza taarifa hiyo ndani ya ukurasa wa Azam FC.

Ngassa amefanikiwa kuibuka mfungaji bora wa ligi kuu Tanzania Bara katika msimu wake wa kwanza wa ligi kuu Tanzania kwa kuifungia Azam FC goli 16.
 




EmoticonEmoticon