MTENDAJI ASWEKWA RUMANDE KWA MATUMIZI MABAYA YA FEDHA ZA UMMA


 Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo(Mbele Kulia) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Longido Mhe. Daniel Chongolo(Mbele kushoto ) wakiwasili  kwenye Mkutano wa hadhara  katika Kijiji cha  Esokonoi.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Londigo, Juma Mhina ameamuru polisi wa Wilaya hiyo kumkamata na kumuweka ndani Mtendaji wa Kata ya Gilai Lumbwa, Paul Lucas baada ya kutuhumiwa kutumia Fedha za umma vibaya
zilizochangwa na wananchi wa maeneo hayo kwa ajili ya kuinua Sekta ya Elimu.
 

Agizo hilo la Mhina lilifanikiwa baada ya mara kwa mara kushindwa kumkamata Paulo baada ya kumkwepa kila alipokuwa akitafutwa na hatimaye mtendaji huyo kujitokeza kwenye Mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisgo Gambo uliofanyika kwenye Kijiji cha IIchang Sapukin kata ya Gilailumbwa.
 
    
Mmoja kati ya wananchi walioshirki Mkutano huo Bi. Anni Mollel alimshukuru Rc Gambo kufika Kijijini hapo na kujionea hali halisi ya ujenzi wa Shuleya Sekondari ambayo wananchi walichanga Fedha zao zaidi ya Tsh Mil 96 ila hazikutumika kama ilivyokusudiwa badala yake viongozi wa Serikali na Wenyeviti wa Kijiji walitumia Fedha hizo kujinufaisha binafsi badala ya kuwasaidia watoto kukaa kwenye mazingira mazuri ili wapate Elimu.


EmoticonEmoticon