KAYA 491 zimeondolewa katika mpango wa kunusuru na umaskini unaotekelezwa na Mfuko wa Taifa wa Jamii (Tasaf), wilayani Same, Mkoa
wa Kilimanjaro, kutokana ukiukwaji wa taratibu wakati wa kuziorodhesha.
Hayo yameelezwa na Mratibu Msaidizi wa TASAF, wilaya ya Same, Habi Msangi wakati wa hafla ya uhamilishaji wa fedha za mradi huo, iliyofanyika katika kijiji cha Marindi, kata ya Miembeni wilayani Same.
Aliongeza, “Tulifanya uchunguzi huo bila upendeleo kwa kushirikisha pande husika na kujiridhisha bila mashaka yoyote na ndipo tukachukua uamuzi huo”.
Aidha alisisitizia dhamira ya mfuko huo ya kuwa unalenga kaya maskini
lengo kuu likiwa ni kuboresha sekta ya afya na ile ya elimu kwa kaya masikini.
Nao baadhi ya wanufaika katika mradi huo, wameipongeza serikali kwa uamuzi wa kuzifuta kaya hizo na kwamba ni sahihi kwa vile zina uwezo kiuchumi.
Kwa upande wake mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Same AnnaClaire
Shija, alisema kuwa kuna malalamiko ambayo aliyapokea kutoka kwa wananchi kuhusu kuwepo kwa kaya zilizoingizwa katika mgao wa Tasaf wakati zinauwezo wa kifedha.
Hata hivyo mkurugenzi huyo aliongeza kusema kuwa kupitia mpango huo umewaza kuzisaidia kaya maskini ambazo zilikuwa hazina uwezo kuwanunulia mahitaji ya shule, ufugaji pamoja na kuwapeleka watoto klinki.
EmoticonEmoticon