WATAALAMU WA UCHUNAJI WAPEWA MAFUNZO


Safina Sarwatt,Moshi,


MAMLAKA ya maendeleo ya biashara Tanzania(TAN TRADE) imetoa mafunzo kwa maafisa mifugo ,wafanyabiashara  pamoja na watalaamu wa uchunaji wa ngozi  katika manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro  lengo likiwa ni kuboresha bidhaa ya ngozi itayokubalika  kwenye soko la dunia.

 Akizungumza kwenye mafunzo hayo mjini Moshi mkoani Kilimanjaro Mkurungenzi wa huduma wa TAN TRADE Tanzania Fidelis Mugenyi amesema  mafunzo hayo yamelenga zaidi katika kuboresha bidhaa ya ngozi.

Amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kujadili kwa pamoja namna ya kuboresha ngozi mbayo itakubalika katika soko la ndani na nje.

Mugenyi amesema kuwa sekta ya ngozi inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uchunaji mbaya wa ngozi ,uandaaji  pamoja uwekaji alama kwenye ngozi  hali inayochangia bidhaa hiyo kukosa ubora unatakiwa .

Amesema kuwa jitihada mbalimbali zakuboresha  ngozi zimeendelea kufaywa ili kuimarisha soko la  biashara ya ngozi ndani na nje ya nchi.

Akizungumza mara baada ya mafunzo hayo mtaalamu wa uchunaji wa  ngozi Wilfred Msele amesema  kuwa tatizo kubwa ni wafanyabishara wa ngozi  wamekuwa  wakiwalangua kwa kuwa wa pangia bei za kununua jambo ambalo linachangia ngozi nyigi kuuzwa kama chakula cha mbwa.

Amesema kuwa ni vema sasa watalamu wa ngozi wakapanga bei na siyo kupangiwa bei na wafanyabiashara na kwamba itasaidia kuongeza ubora wa biadhaa hiyo.

Awali akifunga mafunzo hayo kaimu katibu tawala wa mkoa wa  Kilimanjaro Lidya Riwa amesema kuwa serikali imekuwa ikipoteza mapato mengi yanayotokana na mali ghafi ya ngozi na kwamba mafunzo hayo yatasaidia kuongeza ubora wa bidhaa  nakuogeza pato la mkoa na taifa kwa ujumla.


EmoticonEmoticon