SHULE YA SEKONDARI MANGOTO NA MSINGI LANGASANI ZAPEWA MADAWATI NA TPC




KIWANDA cha sukari cha TPC kilichopo mjini  moshi mkoani  Kilimanjaro,kimekabidhi madawati 100 kwa shule ya sekondari Mangoto  na shule msingi Langasani katika   kata ya  Kahe wilayani moshi mkoani Kilimanjaro.


Akizungumza   wakati akikabidhi madawati  kwa shule sekondari Mangoto  Afisa tawa wa kiwanda cha sukari TPC Jafari Ally amesema kuwa lengo la kampuni ya sukari ni kuisaidia jamii katika masuala mbalimbali za kimaendeleo ikiwemo elimu ,afya na miuondo mbinu ili kuimarisha uhusiano mzuri.

Jafari amesema kuwa kiwanda  hicho kupitia  taasisi yake ya  FT Kilimanjaro, imeona haja  kubwa ya kuchangia elimu  katika harakati za  kampeni  ya kitaifa ya  kumuunga mkono Rais Dkt John Pombe Magufuli ya kuchangia madawati.


Amesema kuwa jumla ya madawati 100 zilizotole na kiwanda hicho ni kufutia upungufu uliopo kwenye shule hizo mbili ambapo kila shule madawati 50.

 

Ally amesema kuwa jumla madawati hayo yamegharimu kiasi cha fedha za kitanzania shilingi million 15.


Nae mwenyekiti wa bodi ya shule ya Mangoto sekondari,Jones Mrindoko ameipongeza kiwanda cha TPC kuona umuhimu huo ya kuchangia madawati kutokana na kwamba kwa kipindi cha zaidi ya miaka mitatu wanafunzi walikuwa wakikaa chini .


Amesema shule ya Mangoto sekondari ilikuwa inakabiliwa na tatizo kubwa ya upungufu wa madawati jambo ambalo ilikuwa ikichangia walimu kulazika kuazima viti kwa majirani.


Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Mangoto,Titho Kithojo amesema kwa sasa shule haina mapungufu ya madawati na kwamba madawati 100 walizopokea zinatosheleza mahitaji ya wanafunzi.


Amesema tatizo kubwa kwa sasa uhaba wa mabara mbili na upungufu wa majengo mawili  madarasa  kutokana na ongezeko kubwa ya mwanafunzi .


Amesema kuwa shule kwa sasa inawanafunzi 320 na kwamba madarasa yaliyopo hatoshelezi .


EmoticonEmoticon