Kipaji ni uwezo ambao mtu huzaliwa nao
(talanta),Talanta hiyo imegawanyika katika makundi mbalimbali na
kumfanya mtu aweze kufikiri, kubuni, kuvumbua au kusanifu kitu fulani,
vilevile kipaji huusisha kwa asilimia kubwa na viungo vya mwili katika
kufanya jambo fulani kama vile ufundi, kucheza na vitu vingine vingi.
Pia
watu wengi hujiuliza kipi kinaanza kati ya ndoto na kipaji? Ukweli ni
kwamba kipaji huanza kisha ndoto kufuata. Kwa mfano leo unaweza ukawa
una kipaji cha kucheza mpira lakini ndoto yako ni kuwa mchezaji mkubwa
wa mpira afrika mashariki na kati.
Pia
ikumbukwe ya kwamba kipaji huwa hawasomei maana ni uwezo ambao mtu
huzaliwa nao mtu, hivyo elimu hutumika kama nyenzo ya kukuza na
kupalilia kipaji hicho.
Zifuatazo ndizo mbinu za kukuza kipaji chako.
1.Tafakari kila unachokiona na kusikiliza.
Hii
ni mbinu bora sana katika suala la ukuzaji wa kipaji chako kwa sababu
ulimwengu wa leo una vitu vingi hivyo ni lazima ujue ni vitu gani
ambavyo unapenda kusikiliza na kukiona zaidi na kuachana na vitu ambavyo
havikusaidii.
Kwa
mfano, kama leo unataka kuwa muigizaji bora wa filamu ni lazima mara
kwa mara upende kutazama filamu za watu mbalimbali pia ni lazima masikio
yako yawe tayari kusikiliza mambo yote ya muhimu yahusuyo masuala ya
filamu.
Vivyo
hivyo kwa kuutazama mfano huo ni lazima ujue ni kipi kwako ni cha
muhimu katika kukupa taarifa sahihi katika ukuzaji wa kipaji chako.
2. Tafuta mtu wa kukuongoza.
Hili
ni tatizo kubwa sana kwa watu wengi, watu wengi wana vipaji ambavyo
vina uwezo mkubwa wa kuibadili jamii na maisha yake kwa kiwango kikubwa,
lakini changamoto kubwa ambayo inawakabili watu hao ni kwamba hawana
mtu sahihi ambaye ana husika kwa asilimia kubwa katika kumuongoza katika
tasnia ambayo anayoifanya.
Watu wengi wanapenda kukomaa peke yao katika vipaji vyao na mwisho wa siku vipaji hivyo hufa.
Inawezekana
ukawa unadhani nazungumzia mtu ambaye anakuvutia ambaye mnafanana
kipaji, la hasha mimi nazungumzia mtu ambaye atakupa ‘network’ ya kukuza
kipaji na hatimaye kutengeneza pesa.
Siku
zote ukumbuke unahitaji mtu sahihi wa kukuongoza na kukisimamia kipaji
chako ili uweze kutimiza ndoto zako, hiyo ni ya muhimu sana kuliko neno
lenyewe.
3. Jiunge katika vikundi mbalimbali.
Ili
uweze kuwa bora zaidi katika kipaji chako huna budi kujiunga katika
vikundi mbalimbali ambavyo vinajihusisha na vitu ambavyo vinalandana na
kipaji chako.
Kwa
mfano, unapenda kuwa mwanamziki bora ni lazima ufuatane na watu wenye
vipaji vya mziki kwani kufanya hivyo ni kujifunza mengi kutoka kwao, pia
ukumbuke ule usemi kutoka kwa wahenga wetu ambao husema penye wengi
pana mengi.
4. Hudhuria semina.
Kama
una amini katika kujifunza, bali endelea kujifunza kwa kuwa karibu na
watu ambao huendesha semina ambazo zinaendana kwa asilimia kubwa na
kipaji chako.
Kufanya
hivi kutakupa hamasa na ufanisi wa kiutendaji ili kuhakikisha ya kwamba
ndoto ya kipaji chako inakwenda kuwa kweli baada ya muda mfupi hasa
pale ambapo utachukua jukumu ya yale uliyojifunza kuyaweka katika
matendo.
5. Kujifunza vitu vipya.
Kujifunza
vitu vipya ndipo ambapo siri ya mafanikio kila mmoja wetu ilipo,
nimesema kujifunza vitu vipya kila kwa sababu ulimwengu wa sasa kila
siku kuna uvumbuzi wa vitu mbalimbali kila itwatayo leo hivyo fanya
makusudio ya dhati kuweza kujifunza.
Hivyo
wito wangu kwako ni uwe karibu sana na vyombo mbalimbali ambavyo
vitakupa taarifa sahihi hususani suala zima la jinsi gani utaweza
kukuza kipaji chako na hatimaye kupata pesa.
Dunia
ni pana, ila ina maneno machache naomba kwa leo niishie hapo tukutane
katika makala iyayo, pia usisite kumshirikisha mwingine kama ambayo mimi
nimeamua kufanya kwako.
EmoticonEmoticon