ROONEY NJE EUROPA LEAGUE


KLABU ya Manchester United imetangaza kikosi cha wachezaji 20 watakaosafiri kwa ajili ya mchezo wao wa Europa League dhidi ya Feyenoord ya Uholanzi, huku Wayne Rooney na Henrikh Mkhitaryan yakiwa miongoni mwa majina ya wachezaji walioachwa.
 
Jesse Lingard ambaye sambamba na Mkhitaryan walitolewa wakati wa mapumziko katika mchezo wa Manchester derby Jumamosi iliyopita pia hatakuwepo, wakati Antonio Valencia akiwa mchezaji mwingine aliyeachwa.
 
Meneja wa United Jose Mourinho tayari ameshathibitisha kuwa Marcus Rashford ataanza katika mchezo huo wakati wachezaji wengine kama Tomothy Fosu-Mensah na Memphis Depay nao pia wakitegemewa kupata nafasi.
 
Mkhitaryan ambaye amekuwa akiripotiwa kutokuwa na furaha Old Trafford kutoka na nafasi anayopangwa, hakuwepo katika mazoezi ya kikosi kilichosafiri kwenda Rotterdam huku Phil Jones akiwa mchezaji mwingine ambaye hakufanya mazoezi.


EmoticonEmoticon