RADIO 5 NA MAJIC FM ZAKUTWA NA HATIA ZAPEWA ONYO KALI NA ADHABU




KITUO cha Redio cha Magic FM  cha jijini Dar es Salaam wamepewa onyo kali na kumwomba radhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, DKT.John Pombe Magufuli, wasikilizaji na wanaanchi kwa ujumla kwa kosa la kukiuka
kanuni za huduma za utangazaji (Maudhui) za 2005.

Amesema kuwa wanatakiwa kuomba radhi kwa siku tatu mfululizo katika taarifa za habari za kuanzia saa kumi jioni hadi saa tatu usiku kuanzia Septemba 17-19 mwaka huu.


Kwa upande wa Kituo cha utangazaji cha Redio 5 cha Arusha kimepigwa faini ya shilingi milioni tano kwa kosa la kukiuka kanuni za huduma za utangazaji (Maudhui) za 2005 kupitia kipindi chake cha Matukio kilichorushwa hewani kati ya saa mbili na saa tatu usiku.

Pia kituo hicho cha Redio 5 kimefungiwa kwa miezi mitatu kuanzia leo, hata hivyo kituo hicho kimewekwa chini ya uangalizi maalumu kwa muda wa mwaka mmoja baada ya kipindi cha Kufungiwa Kumalizika.

Amesema kuwa haki ya kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo iko wazi ndani ya siku 30 kuanzia leo.


EmoticonEmoticon