CHAMA cha walimu (Cwt) Mkoa Wa Kilimanjaro kimebainisha mapungufu
katika zoezi la uhakiki wa walimu,kutokana na zoezi hilo kuchukua
muda mrefu na gharama kubwa ya usafiri ambazo ni sehemu za
mishahara yao.
Akizungumza na mwandishi wa habari mjini Moshi Mkoani humo katibu wa
chama cha walimu (Cwt)mkoa Kilimanjaro,Ally Mbaga amesema kuwa zoezi
hilo limekuwa na mapungu mengi kutokana na kuchukua muda mrefu huko
wanafunzi wakikosa vipindi vingi.
Amesema kuwa zoezi la uhakiki wa walimu limekuwa la mateso kutokana
na walimu kutumia wiki mbili hadi tatu kwa ajili uhakiki ambapo
wanatumia gharama kubwa za usafiri na malazi kwa walimu wanaoishi
sehemu za vijijini ambazo fedha hizo ni sehemu ya mishahara yao.
Amesema maeneo mengi katika mkoa wa Kilimanjaro hadi kufika vituo vya
uhakiki wanalazika kutumia zaidi ya sh.40000 hadi 50000 na ni
vema sasa serikali ikaangalia namna nyingine ya kufanya uhakiki kwa
kuwafuata kwenye vituo vyao vya kazi ili kuondoa adha hiyo.
Mbaga aliendelea kueleza kuwa tatizo la ucheleweshwaji malipo ya walimu
waliopandishwa madaraja katika mkoa Kilimanjaro bado ni changamoto
kwa walimu wengi waliopandishwa madaraja kwa muda mrefu hawajalipwa
hadi sasa.
EmoticonEmoticon