RAIA VIETNAM JELA MIAKA MITATU


MAHAKAMA kuu kanda ya Moshi imehukumu kifungo cha miaka mitatu au
kulipa faini ya shilingi milioni kumi , Raia wa nchini Vietnam, Honang
Trung mwenye umri wa miaka(50), baada ya kukutwa na hatia ya kujaribu
kusafirisha nyara za serikali ambazo ni meno  60 na kucha 261 za
Simba.

Trung alikamatwa na maafisa usalama na kikosi cha kuzuia uhalifu
Disemba  mwaka 2015 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro
(KIA) akiwa na meno hayo ya Simba na Kucha zake vyote vikiwa
vinakadira  kuwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 300 ambapo
alikuwaakisafirisha kwenda  nchini Qatar.

Akisoma hukumu  hiyo  Jaji wa mahakama ya kuu kanda ya Moshi, Aishiel
Sumari, amesema kuwa mtuhumiwa huyo amekutwa na hatia ya kusafisha
nyara za serikali kinyume  cha sheria na kwamba anawajibika kulipa
faini ya shilingi milioni kumi au kwenda jela miaka mitatu.

Amesema mtuhumiwa huyo amekuhumiwa kwa mujibu wa sheria ya uhujumu
uchumi na uhifadhi wa wanyama pori sheria  namba 5 ya mwaka 2009.

Baada ya kusoma hukumu hiyo, Trung aliwashangaza mawakili baada ya
kusimama na kumuomba Jaji Sumari ampunguzie adhabu ya kiwango cha
fedha kinachotokana na faini, kwa kuwa afya yake haipo vizuri na ndugu
zake wapo mbali.

Kufuatia ombi hilo, Jaji Sumari alimwambia Trung, hakuna argument
(majadiliano) kwenye hukumu, unapaswa kulipa na kama huna uwezo huo
unakwenda jela.

Hata hivyo mawakili wa pande zote mbili wakulikubaliana na hukumu hiyo
iliyo tolewa na mahakama hiyo.

Mshitakiwa alikuwa akitetewa na wakili msomi, Wakisa Sambo  huku
upande wa wa Jamuhuri ukiwa na wakali mashuhuri, Eginasi Mwinuka.


EmoticonEmoticon