SIMBA YAONGEZA KIKOMBE KWA MWAKA 2012


Mabingwa wa Tanzania Bara Simba SC jana walitawazwa kuwa mabingwa wa kombe la Urafiki (ujirani mwema) baada ya kuifunga Azam FC kwa mikwaju ya penati 4-3.

Katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, na kushuhudia dakika 90 zikimalizika kwa kufungana goli 2-2, hivyo changamoto ya mikwaju ya penati ikachukuwa nafasi.

Simba walikuwa wa mwanzo kupata goli katika dakika ya 29 mfungaji akiwa Felixs Sunzu, huku Azam FC awakizawazisha goli hilo katika dakika 45 kupitia kwa Khamisi Mcha Viali, aliye ngara vilivyo hapo jana. Na kupelekea kipindi cha kwanza kumalizika kwa sare ya goli 1-1.

Azam FC waliokuwa chini ya kocha msaidizi Kali Ongala hapo jana, walijipatia goli la pili kupitia kwa mfungaji bora wa ligi kuu Tanzania Bara ambaye aliingia kwa mara ya kwanza katika michuano hiyo akitokea benchi John Raphael Boko.

Simba SC walisawazisha goli hilo kupitia kwa kiungo bora kabisa nchini Mwinyi Kazimoto kwa mkwaju wa peanati. Na kupelekea dakika 90 kumalizika kwa sare ya goli 2-2, hivyo mikwaju ya penati ikaipa Simba SC ubingwa wa kombe la Urafiki.

Mshambuliaji wa Azam FC toka Ivory coast Kpre Herman Tchetche ndie aliyeibuka mfungaji bora katika michuano hiyo kwa kufunga goli 5.


EmoticonEmoticon