Azam FC, Simba SC, Yanga na Mafunzo ndizo timu kutoka Tanzania zilizotinga hatua hiyo, huku nyingine zikiwa ni APR ya Rwanda, URA ya Uganda, Atletico ya Burundi na mwalikwa AS Vital ya DR Congo.
Azam FC iliyotinga hatua hiyo kama kinara wa kundi B baada ya kutoa suluhu ya bila kufungana na Tusker iliyokuwa pungufu hapo jana watacheza na Simba SC iliyomaliza ya 3 katika kundi A., baada ya jana kulazimishwa sare ya goli 1-1 na AS Vital iliyomaliza wa kwanza.
Katika mchezo huo wa jana Simba SC walipoteza penati kupitia kwa Felixs Sunzu katika dakika ya mwisho wa mchezo, huku goli lao la kusawazisha likifungwa na Haruna Moshi Boban katika kipindi cha pili.
Yanga walio maliza wa pili katika kundi C watacheza julai 23 dhidi ya Mafunzo iliyomaliza wa pili kundi B.
RATIBA YA ROBO FAINALI KAGAME
JULAI 23
URA Vs APR
YANGA Vs MAFUNZO
JULAI 24
AS VITAL Vs ATLETICO
SIMBA SC Vs AZAM FC
EmoticonEmoticon