BAHANUZI NA TADDY WACHUANA VIKALI UFUNGAJI BORA



Bahanuzi

MSHAMBULIAJI mpya wa Yanga, Said Bahanuzi anachuana vikali na mshambuliaji wa AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Taddy Etikiama katika mbio za kuwania kiatu cha dhahabu kwenye michuano ya Klabu Bingwa ya soka Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame.
 
Bahanuzi, aliyesajiliwa kutoka Mtibwa Sugar msimu huu, ana mabao matano hadi sasa na mpinzani wake ana matano pia, lakini moja alifunga kwa penalti kwenye mechi dhidi ya Simba SC.
 
Hamisi Kiiza ‘Diego’, nyota mwingine wa Yanga kutoka Uganda, anashika nafasi ya pili kwa mabao yake manne, akifuatiwa na Suleiman Ndikumana wa APR matatu, Abdallah Juma ‘Dullah Mabao’ wa Simba SC, Leonel St Preus wa APR, Didier Kavumbagu wa Atletico, Feni Ali na Robert Ssentongo wa URA, wote mabao mawili kila mmoja.
WANAOONGOZA KWA MABAO:
Taddy Etikiama                AS Vita       5
Said Bahanuzi                  Yanga SC    5
Hamisi Kiiza                     Yanga SC   4
Suleiman Ndikumana        APR            3
Abdallah Juma                 Simba SC    2
Leonel St Preus               APR            2
Didier Kavumbagu            Atletico      2
Feni Ali                           URA          2
Robert Ssentongo            URA           2


EmoticonEmoticon