Timu ya taifa ya Zanzibar 'Zanzibar Heroes' imerejea jana kutoka nchini Kurdistan wakiwa wameshika nafasi ya tatu katika michuano ya VIVA Wordcup iliyomalizika juni 9 mwaka huu.
Michuano hiyo ya dunia ilihusisha mataifa yasiyo wanachama wa shirikisho la mpira wa miguu la kimataifa 'FIFA' ambapo mataifa 9 yalishiriki mashindano hayo nchini Kurdistan.
Zanzibar Heroes wameshika nafasi hiyo baada ya kuwachalaza Province ya Ufaransa magoli 7-2 katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu uliochezwa juni 9.
Zanzibar Heroes walikwaana na Province baada ya kufungwa na Cyprus goli 2-0 katika mchezo wa nusu fainali.
Zanzibar Heroes walitinga hatua ya nusu fainali baada ya kushinda goli 6-1 kabla ya kushinda goli 3-0 na kufanikiwa kuingia hatua hiyo wakiwa vinara wa kundi B lililokuwa na timu 3.
Mshambuliaji wa Azam FC Khamis Mcha Viali aliibuka mfungaji bora wa michuano hiyo.
EmoticonEmoticon