TIMU zinazotarajiwa kushiriki michuano ya netiboli Ligi Daraja
la Kwanza mwaka huu zimepewa nafasi ya kusajili nyota si zaidi ya watatu
kutoka nje ya klabu zao.
Ligi hiyo imepangwa kurindima Uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya, kuanzia Septemba 8 hadi 15. Awali mashindano hayo yalipangwa kufanyika Agosti mwaka huu, lakini yamesogezwa mbele kupisha zoezi la sensa ya taifa litakalofanyika mwezi huo.
Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Netiboli Tanzania (CHANETA), Rose Mkisi, alisema wameamua kutoa nafasi hizo tatu, ili kuzipa nafasi timu kusajili wachezaji kutoka nje ya klabu zao kwa lengo la kuongeza ushindani.
Mkisi alisema, cha msingi kinachotakiwa kufuatwa na klabu hizo ni kutosajili zaidi ya nyota watatu katika klabu moja kama ilivyoruhusiwa na CHANETA kitasimama katika sheria na kanuni za mashindano hayo, kwa klabu ambayo itakiuka taratibu.
“Klabu zote zinatakiwa kutuma majina ya wachezaji waliowasajili, ili tuweze kuhakiki na kuwapa vitambulisho ili kuyafanya mashindano haya katika utaratibu mzuri,” alisema Mkisi.
Aliongeza kuwa, timu 20 zinatarajiwa kushiriki michuano hiyo, zikiwemo sita zilizopanda daraja kutoka la pili na kwamba, mashindano hayo kwa mwaka huu wanategemea yatakuwa na upinzani kutokana na timu kongwe na zile zilizocheza ligi hiyo zamani kurejea kwenye ‘chati’.

EmoticonEmoticon