Shirikisho
la Ngumi la Kimataifa na Chama cha Ngumi cha Marekani (IBF/USBA)
limemteua Rais wa Shirikisho hilo katika bara la Afrika, Mashariki ya
Kati na Ghuba ya Uajemi, Mtanzania Onesmo Ngowi kuwa
Mwenyekiti wa Kamati ya kuandaa mkutano wa 30 wa Shirikisho hilo
mwakani ambao unatarajia kufanyika katika jiji la
Berlin nchini Ujerumani kuanzia tarehe 24 hadi 30 Juni mwaka 2013.
Ngowi
alichaguliwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa shirikisho la IBF/USBA
uliomalizika Hilton Hawaiian Village Resort, jinini Honolulu, Hawaii,
Marekani tarehe 2 Juni.
Uteuzi wa Ngowi unafuatia juhudi zake
alizozifanya kuendeleza shirikisho hilo katika bara la Afrika tangu
ateuliwe na Rais wa zamani wa IBF/USBA Robert Lee Sr. mwaka 1999 jijini
New Jersey, Marekani.
Onesmo Ngowi anakuwa mtu wa kwanza kutoka katika
bara la Afrika kushika nyadhifa kubwa katika taasisi ya ngumi duniani na
hii inaisaidia sana Tanzania na bara zima la Afrika kijitangaza vyema
katika nyanja mbalimbali kama vile Utalii na bishara.
Katika Kamati hiyo ya maandalizi kuna wajumbe sita ambao ni, Louis Priluker wa
Marekani, Roberto Rea wa Italia, Lahcen Oumghar wa Uholanzi na Roberto
Ramirez wa Mexico.
Kamati hiyo itafanya shughuli zake katika kipindi
cha mwaka mmoja na itakutana mara 4 kwa mwaka huku Sekretarieti ya Kamati ya
Ngowi itakuwa katika jiji la New Jersey nchini Marekani kuliko makao
makuu ya shirikisho hilo la ngumi duniani.
Mkutano huo uliazimia
kufanya mkutano wa IBF mwaka 2014 katika bara la Asia na mwaka 2015 IBF
itafanya mkutano wake katika bara la Afrika mahali ambapo patateuliwa.
Ngowi amewahimiza
Watanzania ambao wako katika uandaaji wa mikutano kuchangamkia nafasi
hii ambayo itawaleta watalii zaidi ya 1000 nchini toka nchi zaidi ya 200
duniani. Hii ni nafasi ya nadra sana katika biashara na watanzania ni
muhimu wakachangamka kama wenzao wengine katika nchi zinazokuwa wenyeji
wa mikutano kama hii.
EmoticonEmoticon