![]() |
Twiga iliyoondoka nchini Alhamisi na msafara
wa watu 24 wakiwemo wachezaji, benchi la ufundi na viongozi itacheza na
Ethiopia, imepania kufanya vizuri leo, ili kujitengenezea mazingira
mazuri ya kufuzu kwenye Fainali hizo za Nane za Kombe la Afrika kwa
Wanawake (AWC) zitakazofanyika Novemba mwaka huu, Equatorial Guinea.
Baada
ya mechi ya leo, Addis Ababa, timu hizo zitarudiana Juni 16 mwaka huu
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Twiga Stars ikifanikiwa kuitoa
Ethiopia itakuwa imepeta tiketi ya kwenda Equatorial Guinea.
Wachezaji
waliopo Addis na kikosi cha Twiga ni Amina Ally, Asha Rashid (nahodha),
Esther Chabruma, Ettoe Mlenzi, Evelyn Sekikubo, Fadhila Hamad, Fatuma
Bashiri, Fatuma Khatib, Fatuma Mustafa, Fatuma Omari, Maimuna Said,
Mwajuma Abdallah, Mwanahamisi Omari, Mwanaidi Tamba, Mwapewa Mtumwa,
Rukia Hamis, Semeni Abeid na Zena Khamis.
Kwa
upande wa Benchi la Ufundi ni Charles Mkwasa (Kocha Mkuu), Nasra
Mohamed (Kocha Msaidizi), Furaha Francis (Meneja wa Timu), Mwanahamisi
Abdallah (Mtunza Vifaa) na Christina Luambano (Daktari wa Timu).
Twiga
Stars ambayo, Mkuu wake wa msafara huko ni Mwenyekiti wa Chama cha Soka
ya Wanawake Tanzania (TWFA) ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji
ya Shirikisho la SokaTanzania (TFF) itarejea nyumbani Mei 28 mwaka huu
saa 6 mchana kwa ndege ya Ethiopian Airlines.
Katika
mechi mbili za kujipima nguvu kabla ya mchezo huo, Twiga ilifungwa 4-1
na Zimbabwe na 5-2 na Afrika Kusini, mechi zote zikipigwa Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam, lakini makocha wameahidi kufanyia kazi mapungufu
na kusema Watanzania watarajie matokeo mazuri leo.
Mungu ibariki Twiga Stars. Ibariki Tanzania. Amin.
EmoticonEmoticon