Timu ya Taifa 'Taifa Stars' hiyo jana imeshindwa kutamba mbele ya Malawi katika mchezo wa kujipima nguvu kabla ya michezo ya kusaka tiketi ya kombe la dunia mwaka 2014 ambapo Taifa Stars itwakwaana na Ivory Coast na Malawi kuwavaa Waganda.
Katika mchezo wa jana uliochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na mchezo ukimalizika kwa sare ya bila kufungana huku Taifa Stars wakifanya makosa ambayo yange igharimu timu hiyo kama Malawi wangekuwa Makini.
Taifa Stars walicheza kiuwelewano katika kipindi cha kwanza na huku wakitengeneza nafasi chache za kujipatia magoli wakati wa Malawi walionekana kuwa hatari kwa mipira mirefu.
Kipindi cha pili kilikuwa kibaya kwa stars ambapo viungo walipotea na kadri ya dakika zilivyosogea wachezaji walionekana kuchoka.
Nafasi pekee ambayo Stars wameijutia kuipoteza ilikuwa katika dakika ya 58 ambapo Shomari Kapombe na Mbwana Samata waligusiana vyema na mpira wa mwisho kumkuta Samata ambaye aliingia na mpira kwenye eneo la hatari akitokea upande wa kulia na alipo piga pasi ya chini chini kuelekea kwa Haruna Moshi 'BOBAN' ambapo beki wa Malawi ulimgonga na kwenda kugonga mwamba wa pembe ya pili na mpira kuambaa katikati ya Boban na Ngassa kabla ya beki wa Malawi kuutoa nje na kuwa kona.
Pia nafasi pekee ambayo Malawi wanaweza jutia ni ile ya kipindi cha kwanza ambapo Juma Kaseja alielekea hali jojo baada ya Yondan kuhamisha muelekeo mpira katika purukushani ya kuokoa na mpira kumkuta mshambuliaji wa Malawi aliyepiga kichwa na mpira wake kuokolewa na Aggrey Morise.
EmoticonEmoticon