PENGO KUBWA LAONEKANA MSIMBAZI

Aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa Wekundu wa Msimbazi na timu ya Taifa ya Rwanda Patrick Mutesa Mafisango amefariki dunia baada ya kupata ajali ya gari maeneo ya Tazara jijini Dar.

Mafisango amakutana na umauti huo wakati akijaribu kumkwepa mwendesha pikipiki maarufu kama dereva toyo ndipo gari lake likakosa mwelekeo na kujikuta likiingia mtarani na kupoteza maisha yake.

Mafisango kabla ya kujiunga na Wekundu wa Msimbazi alitokea klabu ya Azam fc na pia alishawahi kuichezea Tp Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Patrick Mafisango ameisaidia Simba kunyakua ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom msimu huu kwa kupachika jumla ya magoli 10 huku moja likiwa kwa njia ya penati na kushika nafasi ya sita kwa ufungaji msimu huu.

Pia Mafisango aliwahi kusimamishwa na uongozi wa Simba kwa utovu wa nidhamu lakini baadae aliomba radhi kwa viongozi na kurudishwa kundini kuungana na wachezaji wenzake wa Simba.

Kabla ya kukutwa na umauti huo Mafisango mechi yake ya mwisho kuitumikia Simba ni kwenye michuano ya kombe la Shirikisho dhidi ya Al-ahly Shand ya Sudan na kukosa penati hatimaye timu yake kutolewa kwenye michuano hiyo kwa penati 9 kwa 8.

Bwana ametoa,bwana ametwaa jina lake lihidimiwe.


EmoticonEmoticon