NYOTA WA NBA NCHINI HASHEEM THABIT KUTOA KLINIKI KWA WATOTO WENYE UMRI CHINI YA MIAKA 17

Hasheem Thabeet ataraji kutoa mafunzo ya siku mbili ya kucheza mpira wa kikapu kwa watoto 200 walio chini ya umri wa miaka 17 kwenye  Uwanja wa Don Bosco kuanzia Juni 2 hadi Juni 3.

Thabeet nyota wa NBA anayechezea timu ya Portland Trail Blazers inayoshiriki Ligi ya Kikapu nchini Marekani (NBA) ataongoza kliniki hiyo yenye lengo la kuibua vipaji kwa watoto.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana,Thabeet amesema  mafunzo ya mwaka huu yatakuwa ni tofauti kidogo na yale ya mwaka jana.

“Ninaimani kliniki hii itakuwa tofauti na ile iliyopita kwa sababu watoto wengi wamepata mwamko wa kucheza mpira wa kikapu baada ya kuona mafanikio ya wenzao,”amesema Thabeet.

Kwa upande wake Meneja wa Sprite nchini Warda Kimaro ambao ni wanadhamini wa mashindano hayo amesema baada ya mafunzo hayo vijana hao watakuwa kwenye mpango maalum wa kuendelezwa na kampuni yake.


EmoticonEmoticon