KAULI ILIYOTOLEWA NA BMT,JATA YAANZA KUIFANYIA KAZI

CHAMA cha Judo Tanzania (JATA), kimeanza kukamilisha masharti waliyopewa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT), ambayo ni kupitia upya katiba yao ya zamani, kuifanyia marekebisho na kuitafsiri ili iweze kutumika kwa Watanzania wasiojua lugha ya Kiingereza.

Akizungumza na gazeti nguli hapa nchini la Tanzania Daima hivi karibuni, Katibu Mkuu wa JATA, Innocent Mallya, alisema zoezi hilo limeishaanza kufanyiwa kazi na limefikia hatua ya mwisho kukamilika.

Mbali na sharti hilo, pia viongozi hao walitakiwa kutafuta ofisi za kudumu, zoezi linalodaiwa kukamilika isipokuwa kwa sasa bado zinatafutwa samani ili uongozi uanze kazi rasmi.

Inocent amesema licha ya kujitahidi kutimiza masharti hayo, kwa sasa wanaandaa taratibu na kanuni zitakazowabana viongozi wa JATA, kutelekeza agizo la BMT la kuwataka viongozi kutojiuzulu endapo kutatokea tatizo ndani ya chama.


Mbali na agizo hilo, taratibu hizo zitawabana viongozi kufuata sheria za serikali na BMT wanapopata mialiko ya kushiriki mashindano ya kimataifa na kuachana na tabia ya kuwasafirisha wachezaji kinyume na taratibu.



EmoticonEmoticon