VIGOGO MANISPAA YA MOSHI MIKONONI MWA TAKUKURU KWA UFISADI MILION 269


Safina Sarwatt,Moshi

TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini (takukuru)mkoani
Kilimanjaro,inachunguza tuhuma za ufisadi wa sh.Milioni 269 unaodaiwa
kufanywa na maofisa wa halmashauri ya manispaa ya moshi wanaotuhumiwa
kukodi magari hewa 311 kwa ajili ya uchaguzi mkuu mwaka 2015.

Habari zilizopatikana jana mjini hapa,zimedaia kuwa,maofisa hao
wanadaiwa kughushi namba za magari na mikataba ya ukodishaji wa magari
kuonyesha kuwa magari hayo yalitumika katika uchaguzi huo  mkuu.

Kamanda wa takukuru mkoani Kilimanjaro,Alex  Kuhanda,alikiri jana
kuwepo na uchunguzi huo lakini hakuwa tayari kuzungumzia kwa undani
kutokana na kubanwa na kanuni na maadili yanayokataza kutoa taarifa za
tukio liliko  kwenye hatua ya uchunguzi.

Kuhanda aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa,atatoa taarifa za
uchunguzi wa tuhuma hizo mara baada ya uchuguzi kukamilika pamoja na
hatua ambazo zitachukuliwa na taasisi yake kwa maofisa watakaobainika
kuhusika katika tuhuma hizo.

Uchunguzi uliofanywa na Mtanzania,umebaini kuwa,miongoni mwa magari
hayo hewa,18 imebainika ni pikipiki ambazo hata hivyo zimesajiliwa na
wamiliki wake wanaishi mikoa ya nyanda za juu kusini na kulingana na
uchunguzi wa takukuru,wamiliki wa pikipiki hizo hawajawahi kufika
mjini moshi.

Kwa mjibu wa uchunguzi wa gazeti hili,kati ya mgari hayo hewa,13
yalikuwa yakilipiwa sh,Milioni 6 kwa kila gari katika muda wote wa
shughuli za uchaguzi huku mengine yakipiliwa sh,300,000 kila moja kwa
siku .


Mbali na kukodi magari hewa,maofisa hao pia wanatuhumiwa kughushi
mikataba kuonyesha kuwa wamiliki wa mgari hiyo walilipwa pesa hizo na
hivyo kuwawezesha kujiingizia mamilioni ya fedha kwa njia za
udanganyifu.

Naye mkurugenzi wa  manispaa ya Moshi,Michael Mwandezi,jana alikiri
kuwepo kwa uchunguzi unaofanywa na maoifa wa takukuru dhidhi ya
maofisa wa manispaa hiyo lakini alikataa kuzungumzia uchuguzi huo na
kuomba suala hilo liachwe kwenye vyombo vya uchunguzi.

Wakati maofisa hao wakichunguzwa,ofisa mwandamizi ofisi ya mkuu wa
mkoa wa Kilimanjaro ambaye ni katibu tawala msaidizi,Grace
Makiluli,naye ameingia matatani akituhumiwa kughushi nyaraka za malipo
na kufuja sh,Milioni 4 ambazo ni malipo ya posho za wasimamizi
wasidizi wa uchaguzi mkuu mwaka 2015.

Taarifa zilizopatikana jana mjini hapa,zimedaiwa kuwa,ofisa huyo
anadaiwa kughushi nyaraka na saini za watumishi wa serikali ambao
walikuwa wamepangiwa majukumu katika kusimaia uchaguzi huo na hadi
sasa hawajalipwa posho hizo.

Kamanda wa takukuru mkoani Kilimanjaro,Alex Kuhanda,pamoja na kukiri
kuwepo kwa uchunguzi huo alikataa kuzungumzia kwa undani kutokana na
suala hilo kuwa mikononi mwa maofisa wa taasisi yake kituo cha Holili
kilichopo wilaya ya Rombo.

Hata hivyo ofisa huyo jana alikana tuhuma za kuhojiwa na Takukuru
alipozungumza kwa njia ya simu na waandishi wa habari wakti katibu
tawala (RAS)mkoa wa Kilimanjaro,Injinia Aisha Amour akigoma kujibu
swali aliloulizwa na waandihi wa habari juu ya ofisa wake kuhojiwa na
takukuru.


EmoticonEmoticon