Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kuwaua
majambazi wanne waliokuwa wamejichimbia katika pori la Mbande jijini Dar
es Salaam mara baada ya mapigano makali na majibizano ya risasi
yaliyojiri kwa zaidi ya dakika arobaini.
Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Kamanda wa
Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Simon Siro, amesema kuwa jeshi la
Polisi limefanikiwa kumkamata mmoja wa Majambazi aliyehusika na tukio la
ujambazi CRDB Mbagala
"Polisi mara baada ya kumkamata mtuhumiwa huyo alikiri kuhusika na tukio
hilo akiwa na wenzie saba hivyo aliwaambia askari kuwa anawapeleka
sehemu walipo wenzake kwenye pori la Dondwe ambapo wanafanya mazoezi ya
kivita.
"Walipofika katika eneo hilo la mipakani Chanika ghafla majambazi hayo
yalianza kufyatua risasi kwenye uelekeo wa askari na mtuhumiwa alikimbia
na askari wakaanza kujibu mashambulizi na askari wakafanikiwa kujeruhi
majambazi wanne na kufanikiwa kupata bunduki ya kijeshi aina ya SMG
iliyofutwa namba za usajili ikiwa na risasi 22 ndani ya Magazine..," amesema Siro.
Amesema kuwa majeruhi hao walikimbizwa hospitali ya Taifa Muhimbili na
wakati wanapatiwa matibabu wote kwa bahati mbaya walifariki Dunia
kutokana na majeraha ya risasi.
Ameongeza kuwa uchunguzi huo umebaini kuwa Bunduki hiyo ni moja ya zile zilizoporwa wakati askari wakibadilishana lindo.

EmoticonEmoticon