TRA MKOA WA ARUSHA WAGAWA MAFUTA JESHI LA MAGEREZA

Madumu ya mafuta yaliyotolewa na TRA

Madumu ya mafuta yaliyotolewa na TRA

Madumu ya mafuta yaliyotolewa na TRA
Mamlaka ya mapato nchini TRA mkoa wa Arusha imegawanya jumla ya lita 8180 za mafuta ya taa kwa jeshi la magereza,mafuta ambayo yalikamatwa Namanga yakiingizwa nchini kinyume cha sheria yakiwa na thamani ya shilingi milion nne, laki tisa na elfu nane.

Akizungumzia kugawanywa kwa mafuta hayo meneja wa TRA mkoa wa Arusha ndugu Apili Mbaruku ameeleza kuwa mafuta hayo yaliyo gawnywa yalikamatwa eneo la Namanga yakiingia nchini isivyo halali wakiwa wanafanya ziara ya kawaida na kuelezea kuwa wameamua kugawa mafuta hayo kwa jeshi hilo la magereza kutokana na kuwa na uhitaji mkubwa.

 Tokea January 2016 hadi Septemba waliweza kukamata bidhaa zenye thamani ya sh milion 568.1, Katika makabidhiano hayo ya mafuta ya taa kwa jeshi la magereza mwakilishi wa mkuu wa magereza mkoa wa Arusha Inspecta Silivesta ameshukuru msaada huo walio patiwa na kueleza kuwa mafuta hayo watakuwa wanatumia pindi umeme unapokatika.


EmoticonEmoticon