SOUTHAMPTONYAVUNJA REKODI YAKE KWA KUMSAJILI BOUFAL


Klabu ya Southampton imevunja rekodi yake yenyewe kwa kumsajili kiungo wa kimataifa wa Morocco Sofiane Boufal kutoka klabu ya Lille ya Ufaransa kwa kitita cha paundi milioni 16. Boufal mwenye umri wa miaka 22, amefunga mabao 11 msimu uliopita na kuisaidia Lille kumaliza katika nafasi ya tano katika Ligue 1 na kufuzu michuano ya Europa League.

Rekodi iliyokuwepo kwa Southampton ya kusajili mchezaji ghali ilikuwa ni paundi milioni 15 waliyomnunulia mshambuliaji wa Roma Dani Osvaldo mwaka 2013. Akihojiwa mara baada ya kukamilisha usajili huo, Boufal amesema klabu hiyo ni bora na anadhani itakuwa mahali pazuri kwake kukua zaidi kisoka.


EmoticonEmoticon