Mkuu wa usalama barabarani kanda maalum ya Dar es salaam (ZTO) ACP Awadhi Haji akitoa elimu kwa madereva wa bodaboda waliopo kituo cha daladala cha Tegeta mapema leo, akiwataka wafuate sheria za usalama barabarani ikiwemo kuvaa kofia ngumu pamoja na abiria wao,kwani wasipovaa Kofia ngumu watachukuliwa hatua Kali za kisheria ikiwemo kupelekwa mahakamani.
Vilevile amewataka kutojihusisha na vitendo vya kihalifu wakiwa na pikipiki zao na akawataka madereva hao wawe wasafi pindi watoapo huduma kwa wananchi.
EmoticonEmoticon