KLABU za Chelsea na Everton
zimetajwa kumtaka Kalidou Koulibaly, huku beki huyo akitaka kuondoka Napoli kwa
mujibu wa wakala wake. Wiki iliyopita taarifa zilizagaa kuwa beki huyo mwenye
umri wa miaka 25 alitolewa ofa ya kwenda Arsenal, ingawa Arsene Wenger alikataa
kiasi cha euro milioni 45 kilichohitajika.
Everton na Chelsea zimekuwa
zikimuwinda Koulibaly kipindi hiki cha usajili na wakala wa nyota huyo wa
kimataifa wa Senegal, Bruno Satin amethibitisha mteja wake anaweza kwenda Ligi
Kuu.
Bruno amesema Jumamosi iliyopita walikutana na kujaribu juu ya kuongezewa
mkataba mpya, hata hivyo hawakufikia muafaka kwani madhumuni makubwa ya
mchezaji huyo ni kuondoka na sio kuongeza mkataba.
Wakala huyo aliendelea kudai
kuwa Napoli imekuwa ikisema Koulibaly ni mchezaji mkubwa lakini wamekuwa
hawalioni hilo katika ofa yao ya mkataba mpya.
EmoticonEmoticon