MSHAMBULIAJI nyota wa
klabu ya Manchester United, Wayne Rooney amekataa tena kuanza mazungumzo
na klabu hiyo juu ya mkataba wake mpya.
Nyota huyo na wawakilishi wake
wamekataa pia kuzungumza masuala ya kuongeza mkataba mwingine baada ya
huu kumalizika msimu ujao.
Kuna tetesi kuwa nyota huyo amekataa kusaini
mkataba mwingine kwasababu bado ana nia ya kutaka kuondoka katika klabu
hiyo.
Rooney ameanza msimu huu akiwa katika kiwango cha juu ambapo
amefunga mabao nane katika mechi 13 za Ligi Kuu alizocheza katika kikosi
cha United kinachonolewa na David Moyes.
EmoticonEmoticon