
Jaji Warioba ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Rasimu ya Katiba Mpya katika tukio la kihistoria nchini Tanzania.
"Imependekezwa kwamba matokeo ya Rais yatashikiwa mahakamani lakini kwa masharti," amesema Jaji Warioba hivi punde.
Jaji
Warioba ametaja masharti hayo ni kwamba wagombea wa urais ndio watakuwa
na haki ya kuhoji matokeo ya rais na si vinginevyo. Pili, matokeo hayo
yanatakiwa kuhojiwa ndani ya mwezi mmoja tu na si vinginevyo.
Amesema
pia tume imependekeza kuwapo kwa wabunge wa aina mbili ambao ni wabunge
wa kuchaguliwa na wabunge wengine wa kuteuliwa na Rais.
Pia
amesema kwamba kutakuwapo kwa utaratibu wa wanawake kugombea katika
majimbo. Kwa maana hiyo hakutakuwapo wabunge wa Viti Maalumu.
Pamoja
na hayo, tume ya jaji Warioba imependekeza kuwepo kwa serikali tatu
ambazo ni -serkali ya zanzibar, ya tanganyika na ya muungano.
mambo ya muungano yaliyopendekezwa:
1)katiba ya jamhuri ya muugano wa tanzaia
2)sarafu na benki kuu
3)mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa
4)ushuru
5)ulinzi na usalama
6)usajili wa vyama vya siasa
7)uraia na uhamiaji
EmoticonEmoticon