MTIBWA SUGAR YAWALIZA BILA HURUMA NDUGU ZAO POLISI MOROGORO


Timu ya Mtibwa Sugar imeanza vyema michuano ya Kombe la BancABC Super 8 baada ya kuifunga Polisi, zote za Morogoro mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Ushirika mjini Moshi, Kilimanjaro.
Mabao ya Mtibwa Sugar, inayofundishwa na mchezaji wake wa zamani, Mecky Mexime yalitiwa kimiani na Vincent Barnabas dakika ya 39 na Yussuf Bida dakika ya 49, wakati la Polisi lilifungwa na Nicholas Kabipe mapema tu dakika ya 10.
   
Mechi hiyo ilipangwa kufanyika kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha, lakini Menejimenti ya Uwanja huo ilizizuia timu zikiwa getini na kudai hawana taarifa za mashindano hayo.
Ilielezwa mechi hiyo ingechezwa kwenye Uwanja wa General Tyre mjini hapa, badala ya Sheikh Amri Abeid, lakini imeshindikana na kuchezwa Moshi.

Michuano hiyo ina makundi mawili, ikishirikisha timu nane, Kundi A likiwa na timu za Simba, Jamhuri, Zimamoto na Mtende FC, wakati Kundi B kuna Super Falcon, Azam FC, Mtibwa Sugar na  Polisi Moro na bingwa wa michuano hiyo inayodhaminiwa na Bank ABC ataondoka na Sh. milioni 40, mshindi wa pili Sh. milioni 20, wa tatu Sh. milioni 15 sawa na wa nne, wakati washiriki wengine wataondoka na Sh. Milioni 5 kila moja.
Michuano itachezwa katika vituo vinne vya Dar es Salaam, Zanzibar, Arusha ambako imekataliwa na Mwanza, ambapo timu zitasafirishwa kwa ndege kwenda kucheza mechi katika vituo vyote.

Kila timu itacheza mechi  katika vituo vitatu tofauti,Simba baada ya kutoa sare, itakwea pipa kwenda Arusha kucheza dhidi ya Mtende FC Alhamisi na itasafiri kwenda Mwanza kwa ajili ya mechi yao ya mwisho ya Kundi A dhidi ya Zimamoto Jumamosi.


EmoticonEmoticon