MANJI KUUNDA KAMATI MPYA YANGA

Yusuf Manji
 
Baada ya kuapishwa, viongozi wa Yanga walifanya kikao cha Kamati ya Utendaji, ambacho kilifikia uamuzi wa kuvunja Kamati zote ndogondogo ili kuunda Kamati mpya.

Mwenyekiti wa Yanga, Yussuf Manji alisema Kamati ambayo haitaguswa ni Kamati ya Uchaguzi pekee, iliyo chini ya Mwenyekiti Jaji John Mkwawa.
 
Baada ya kikao cha Kamati ya Utendaji, Manji alifanya kikao kingine kidogo na wanachama, akiwa na Makamu wake, Clement Sanga.
 
Kutoka hapo, Katibu wa Yanga, Celestine Mwesigwa akaenda kuzungumza na Waandishi wa Habari, kuwapa yaliyofikiwa kwenye Kamati ya Utendaji.
 
Waliohudhuria kikao cha Kamati ya Utendajii, pamoja na Mwenyekiti na Makamu wake, wengine ni Wajumbe wa Kamati hiyo, George Manyama, Aaron Nyanda, Mohamed Bhinda, Titus Osoro, Sarah Ramadhan na Mussa Katabaro.

Alikosekana Abdallah Bin Kleb pekee, ambaye yupo Kigali, Rwanda kwa majukumu ya klabu.


EmoticonEmoticon