![]() |
PONGEZI KWAKO; Kocha mpya Taifa Stars, Kim Poulsen kazi ya mwezi uliopita imezaa matunda |
TANZANIA imependa kwa nafasi 12 kwenye orodha ya viwango vya
ubora ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) iliyotolewa leo (Julai 4 mwaka
huu) na shirikisho hilo.
Kwa viwango vya Juni mwaka huu, timu ya taifa ya Tanzania, Taifa
Stars inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, ilikuwa namba 139
hivi sasa imefika nafasi ya 127 ikiwa na pointi 253 kulinganisha na 214 za Juni
mwaka huu.
Timu hiyo ilikuwa katika nafasi hiyo hiyo kwa viwango vilivyotolewa Juni 6 mwaka huu. Hispania ambao ni mabingwa wa Ulaya na Dunia ndiyo wanaoendelea kuongoza kwa kukamata nafasi ya kwanza wakiwa na pointi 1,691.
EmoticonEmoticon