Ezekiel Kamwaga-akiongea na waandishi wa habari
Klabu ya soka ya Simba ya jijini Dar es Salaam inataraji kufanya sherehe kubwa baada ya kutwaa ubingwa wa soka wa Ligi Kuu ya Vodacom katika Ukumbi wa Taifa wa Burudani wa Dar Live siku ya Jumapili Mei 27.
Akiongea na waandishi wa habari Ofisa Habari wa klabu hiyo, Ezekiel Kamwaga, amesema kuwa wameamua kufanya sherehe hizo ndani ya ukumbi huo kutokana na ubora wa ukumbi huo wa Dar Live.
Aidha Kamwaga amesema kuwa siku hiyo pia watawatambulisha wachezaji wapya waliosajiliwa kwa msimu ujao wa ligi hivyo kuwataka wapenzi wa Simba na wananchi wengine kujitokeza kwa wingi siku hiyo ya sherehe.
Kwa upande wake nahodha wa timu hiyo Juma Kaseja amesema haijawahi kutokea kwa klabu yoyote ya Tanzania kufanya sherehe baada ya kuchukua ubingwa,hivyo wanataka watembeze kombe hadharani kama walivyofanya Chelsea baada ya kuchukua Uefa Champion league.
Juma Kaseja-Nahodha
EmoticonEmoticon