SHIRIKISHO la Soka Tanzania(TFF) limeweka wazi kwamba aliyekuwa kocha wa
timu ya taifa(Taifa Stars)Mdenmark Jan Poulsen hatalipwa mishahara yake ya
miezi mitatu iliyosalia katika mkataba wake.
Msimamo huo wa TFF umekuja wiki iliyopita bada ya Poulsen kulilalamikia
shirikisho hilo kwa kutomlipa mshahara wake wa mwezi mmoja,sambamba na fidia
inayotokana na kuvunjwa kwa mkataba wake.
Hivi karibuni TFF ilisitisha huduma ya Poulsen kwa Taifa Stars na badala
yake ikamtangaza aliyekuwa kocha wa timu za taifa za vijana, Kim Poulsen
kuchukua jukumu hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alisema
kuwa hatua ya kutomlipa Poulsen mishahara ya miezi mitatu inatokana ukweli
kwamba kocha huyo hatakuwa na kazi ya kufanya katika kipindi hicho cha miezi
mitatu ya mkataba wake kilichosalia hadi Julai 30.
"Kwanza kabisa ieleweke kwamba kwamba serikali ndiyo iliyokuwa inamlipa Poulsen mshahara baada ya kuingia naye
mkataba na sio TFF."Katika utaratibu wa kawaida wa serikali tunaoufahamu
awezi kulipwa mshahara wa bure wakati hajafanya kazi yoyote,huo ndio ukwli
wenyewe,"alisema Wambura
Akifafanua zaidi, Wambura alisema TFF iliamua kusitisha huduma za Poulsen
licha ya kwamba mkataba wake unaendelea kuwa hai kwa lengo la kutoa nafasi kwa
kocha mpya kupanga mipango ya muda mrefu.
"Kila baada ya muda fulani kocha anatakiwa awasilishe ripoti ya timu
yake,sasa utapataje ripoti sahihi wakati kesho kutwa mkataba wake unamalizika.
"Pia niweke vizuri hapo,TFF haikuvunja mkataba wa Poulsen bado upo na
utamalizika Julai 30 tulichokifanya ni kuzungumza nae na kukubaliana kwamba
hakutaongeza mkataba hivyo tunatafuta kocha mwingine,"alisema.
Wambura aliongeza kuwa,licha ya kibarua cha kocha huyo cha kuinoa Taifa
Stars kusitishwa,bado TFF itaendelea kuwa nae katika mkataba mwingine
unaohusiana na ukufunzi wa makocha nchini.
"Poulsen pia alikuwa na kazi nyingine ya ukufunzi wa makocha hata hapa
ametuaga anakwenda kwao kuhudhuria harusi ya mtoto wake akirudi
ataendelea,"alisema Wambura
Kwa upande mwingine kusitishwa kwa
kibarua cha Poulsen kunahusishwa na
shinikizo la wadau wa soka waliotaka mabadiliko katika benchi la ufundi
kufuatia Taifa Stars kuporomoka
mfululizo kwa takribani miezi saba kwenye viwango vya ubora vya Shiriki
EmoticonEmoticon