Msafara wa wachezaji wa
Simba pamoja na baadhi ya viongozi wao wa benchi la ufundi ulianzia mchana
makao makuu ya klabu hiyo mtaa wa Msimbazi na kupita mitaa mbalimbali ya Dar es
Salaam na kisha kuelekea ukumbi wa Dar Live, Mbagala ambako umati mkubwa
ulijitokeza.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ amesema klabu yake haina mpango na wachezaji Ferick Walulya wa Uganda na Gervais Kago wa Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Amesema wachezaji hao mikataba yao imeisha, hivyo Simba haitahitaji kuwaongezea na kwamba watakuwa huru kujiunga na timu nyingine wanayoihitaji.
Akizungumzia vipaumbele katika usajili wa mwaka huu, amesema Simba ina mikakati ya kuboresha zaidi usajili katika safu ya beki wa kati.
Pia amesema wanahitaji kupata mrithi wa kiungo mahiri wa timu hiyo aliyefariki hivi karibuni kwa ajali ya gari, Patrick Mutesa Mafisango.
Ameongeza kuwa klabu yake imejipanga kuhakikisha kuwa usajili wa mwaka huu unafanyika kiumakini zaidi huku akisisitiza kuwa nguvu pia itawekwa katika kuwasajili wachezaji wa kikosi cha vijana cha timu hiyo.

Simba jana iliandaa
sherehe ya kujipongeza kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa
mwaka 2011/2012.
Hata hivyo baadhi ya wachezaji nyota wa Simba hawakuwepo katika msafara huo kutokana na wengine kuwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzanai ‘Taifa Stars’ kinachojiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Ivory Coast Jumamosi.

EmoticonEmoticon