VIFO VYA WATU WANNE KUNYONGWA




MAITI TAKRIBANI NNE ZIMEKUTWA BARABARANI KATIKA ENEO LA KILALA NDURUMA HUKO TENGERU WILAYANI ARUMERU ARUSHA,

       MAITI HAO WAMEFAHAMIKA KWA MAJINA YA LAIZER NAVABA,JUMBE SAITOTI,ELIAS LOTINGIDWAKI NA RICHARD MAOMBI WOTE WAKAZI WA SOMBETINI ARUSHA

       IMEELEZWA KUWA WATU HAO WAMEKUTWA WAMEUAWA KWA KUNYONGWA HUKU WAHUSIKA WA TUKIO HILO BADO HAWAJAJULIKANA NA  MAITI HIZO NI WANAUME WOTE HUKU MMOJA AKIONEKANA NA UVIMBE KICHWANI.

         KWA TAARIFA AMBAZO TUPO NAZO KWA MUJIBU WA WANANCHI WA SOMBETINI WAMESEMA WATU HAO NI MAJAMBAZI HIVYO WAO NDO WAMEWAUUA KWA KUWANYONGA NA KWENDA KUWATUPIA HUKO TENGERU WILAYANI ARUMERU.

       HIVI SASA JESHI LA POLISI MKOANI ARUSHA LIKIONGOZWA NA ANDENGENYE LIMEKAA KUZUNGUMZIA TUKIO HILO NA MAITI ZIMEHIFADHIWA HOSPITALI YA MKOA YA MOUNT MERU ARUSHA.

       PIA JESHI LA POLISI LIMEWAOMBA WANANCHI KWENDA HOSPITALI HAPO KUWEZA KUWATAMBUA WATU HAO WANAOSADIKIWA NI MAJAMBAZI WALIOUAWA NA WANANCHI WA SOMBETINI.

       KWA MUJIBU WA MWANDISHI WETU ALIYEPO ENEO LA TUKIO HIVI SASA AMESEMA MAITI MOJA IMETAMBULIWA NA MTU MMOJA AMBAE HAKUTAKA JINA LAKE LITAJWE NA KUSEMA ANAMJUA KWA SURA TU HAMJUI JINA NA ANA MKUMBUKA WAKATI WAKIFANYA KAZI PAMOJA MIAKA YA NYUMA.

         TUTAWAJUZA ZAIDI KUHUSU KIKAO AMBACHO KINAENDELEA HIVI SASA CHA JESHI LA POLISI MKOA WA ARUSHA.


EmoticonEmoticon